10 Aprili 2025 - 19:52
Source: Parstoday
Ansarullah yaitahadharisha Marekani kuhusu vita vya nchi kavu dhidi ya Yemen

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullh ya Yemen amelaani mashamulizi ya anga ya Marekani nchini humo na kutahadharisha kuhusu hatua yoyote ya kijeshi ya nchi kavu ya Washington dhidi ya Yemen.

Muhammad al Bukhaiti amesema mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen yamegonga mwamba katika kutimiza malengo iliyoyakusudia na akasema" mashambulizi hayo yamefeli kuwalenga viongozi wa ngazi ya juu wa Ansarullah. 

"Matokeo pekee ya hujuma hizo za Marekani ni kuwauwa raia wasio na hatia", amesema mjumbe huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah. 

Al Bukhaiti ametahadharisha kuhusu hatua yoyote ya uvamizi wa kijeshi wa nchi kavu dhidi ya Yemen na kuongeza kuwa: "Tunawaonya Wamarekani kwamba watakabiliwa na jibu gumu na kali sana iwapo wataingia katika vita vya nchi kavu, iwe moja kwa moja au kupitia vikosi vyao vya niaba ndani ya Yemen." 

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kuwa: "Hata kama makubaliano yatafikiwa kati ya Marekani na Iran, msimamo wa Yemen katika kuitetea Gaza hautabadilika, na tutaendelea kwa uhuru kuiunga mkono mkono Palestina na kuupinga utawala wa Kizayuni wa Israel bila kuathiriwa na hatua za kidiplomasia za kimataifa."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha